Benki ya Dunia yasitisha ufadhili Uganda kisa sheria ya kupinga ushoga

UGANDA, Kampala: Benki ya Dunia imesitisha ufadhili wowote mpya kwa miradi nchini Uganda, ikitaja ukiukwaji wa haki za binadamu kutokana na kupitishwa kwa sheria ya kupinga ushoga.

Taarifa kutoka Benki hiyo inasema ufadhili zaidi unasitishwa hadi mamlaka nchini Uganda itoe sera ya kutosha ya kuwalinda walio wachache, wakiwemo watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na makundi mengine ambayo kwa kawaida yanaainishwa kama LGBTQ+.

“Sheria ya Kupinga Ushoga ya Uganda kimsingi inakinzana na maadili ya Kundi la Benki ya Dunia. Tunaamini maono yetu ya kutokomeza umaskini katika sayari inayoishi yanaweza tu kufanikiwa ikiwa itajumuisha kila mtu bila kujali rangi, jinsia au jinsi,” WB ilisema kwenye taarifa Jumanne.

“Sheria hii inadhoofisha juhudi hizo. Kujumuika na kutobaguliwa ndio msingi wa kazi yetu duniani kote.”

Mwezi Mei, Rais Yoweri Museveni alitia saini na kuwa sheria Sheria ya Kupambana na Ushoga, ikitoa adhabu kubwa kama hukumu ya kifo kwa “ushoga uliokithiri.” Sheria imeleta shutuma kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na nchi za Magharibi kama vile Marekani ambao walitishia vikwazo. Marekani ni mbia mkuu katika Benki ya Dunia.

Benki ya Dunia ilisema imekuwa ikishinda Kampala kutafakari upya sheria hiyo.

Timu kutoka Benki hiyo, ilisema, imekuwa ikizungumza na maafisa wa Uganda kuhusu “hatua za ziada ambazo ni muhimu kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vyetu vya mazingira na kijamii.”

“Lengo letu ni kulinda walio wachache wa jinsia na kijinsia dhidi ya ubaguzi na kutengwa katika miradi tunayofadhili. Hatua hizi kwa sasa zinajadiliwa na mamlaka. Hakuna ufadhili mpya wa umma kwa Uganda utakaowasilishwa kwa Bodi yetu ya Wakurugenzi Watendaji.

Mahusiano ya jinsia moja ni haramu nchini Uganda, hata kabla ya sheria hii, chini ya kanuni ya zamani ya adhabu.

Habari Zifananazo

Back to top button