BENKI ya Stanbic inashikilia nafasi ya nne kwa ukubwa nchini kutokana na kuwaunganisha wateja ikiwemo vijana sanjari na kuwezesha mtangamano wa huduma za kifedha katika kupunguza tofauti za kiuchumi ikiwemo uwezeshwaji wa watu waliopo pembezoni.
Akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya Azaki Jijini Arusha ,Mkuu wa Kitengo cha Sekta za Umma wa benki hiyo,Doreen Dominic amesema benki hiyo ipo mstari wa mbele kuwezesha mtangamani wa huduma za kifedha , kupunguza tofauti za kiuchumi na kuwezesha watu waliopembezoni kujumuishwa kiuchumi .
Amesema benki hiyo imekuwa bega kwa bega kufanya kazi kwa bidii ili kuunganisha huduma zao na mahitaji ya mashirika ya kiraia
Amesisitiza benki hiyo inaamini kubwa teknolojia sio chombo tu bali ni chachu ya mabadiliko na wataendelea kufanya kazi na asasi za kiraia ili kuongea uwezo wao na kuketa matokeo chanya kwa jamii.
Naye Diwani wa Kata ya Ngarenaro,Isaya Doita akifungua mkutano huo kwa niaba ya meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqe ,ametoa rai kwa vijana kutumika mitandao ya kijamii kwa ajili ya kupata fursa za kujikwamu kiuchumi na kujipatia kipato kutokana na teknolojia zinazokuwa kwa sasa badala ya kuitumia vibaya