Benki yazindua akaunti maalum ya walimu

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Akaunti ya Mwalimu kwa lengo la kutoa suluhisho la huduma za kifedha zenye gharama nafuu kwa kundi hilo.

Akaunti hiyo ya kibunifu inalenga kutoa faida na huduma maalum zilizobuniwa kwa ajili ya mahitaji ya kipekee ya walimu na kuwawezesha kufanikiwa kuatua changamoto mbali mbali za kifedha.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo, mkuu wa fedha na masoko ya kigeni, Juliana Mwapachu amesema “Akaunti ya Mwalimu” ni sehemu ya safari ya kujumuisha kifedha na kuwawezesha walimu.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha bidhaa na wateja binafsi, Abel Kaseko alisema: “Akaunti ya Mwalimu ni suluhisho la benki la kipekee lililobuniwa kwa ajili ya walimu nchini Tanzania.

“Inatoa huduma kamili ya bidhaa na huduma za kifedha zilizobuniwa kwa mahitaji ya jamii ya walimu, ikitoa udhibiti mkubwa wa fedha zao na fursa ya kujenga mustakabali imara.”

Kupitia ushirikiano wa NBC na Samsung, walimu watapata punguzo la hadi asilimia 10 katika ununuzi wa kifaa chochote kutoka maduka ya Samsung. Pia kuna punguzo lingine la hadi asilimia 15 katika ununuzi wa paneli za nishati ya jua na pikipiki.

“Akaunti ya Mwalimu inalenga kubadilisha uzoefu wa benki kwa walimu kwa kutoa faida zifuatazo. Hakuna ada ya kila mwezi, tunaelewa umuhimu wa urahisi na matumizi rahisi kwa walimu, hivyo tumefuta ada yoyote ya matunzo yanayohusiana na akaunti hii,” alisema Kaseko.

Mkuu huyo wa kitengio cha wateja binafsi aliongeza: “Ada ya shughuli iliyowekwa: Bila kujali kiasi cha shughuli au njia iliyotumika, walimu watapata ada iliyowekwa ya Sh 2,000 tu kwa aina zote za shughuli, kutoa uwazi na gharama nafuu.”

Habari Zifananazo

Back to top button