Benzema ahusishwa Al-Ittihad

IMERIPOTIWA ombi rasmi kutoka Al-Ittihad kwenda Real Madrid limewasilishwa kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema kuelekea Uarabuni.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Benzema atalipwa €100m kwa mwaka. Makaratasi ya ombi hilo yamewasilishwa wiki iliyopita kabla ya mchezo wa Madrid na Sevilla.

Amesema kuwa Benzema anatamani uhamisho huo ukamilike, hata hivyo anajiandaa kutoa kauli yake kuhusu uhamisho huo.

Advertisement

Real Madrid wamekubali kumpa Benzema mkataba wa mwaka mmoja lakini mshambuliaji huyo hajasaini mpaka sasa.