Biden atua Israel

Rais wa Marekani, Joe Biden amewasili Israeli leo na kupokewa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu.

Kuwasili kwa Biden huko Tel Aviv kulionesha uungaji mkono wake wa nguvu zaidi kwa Israeli tangu shambulio la Oktoba 7 la Hamas ambalo lilisababisha Waisraeli 1,400 na Wamarekani kadhaa kuuawa.

Wamarekani wengine, pamoja na Waisraeli wengi, pia wanashikiliwa mateka na Hamas. Na takribani watu 3,000 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu mapigano yaanze, Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza ilisema Jumanne.

Kuwasili kwa kiongozi huyo kunakuja baada ya jana Hospitali ya Al-Ahli Baptist huko Gaza kulipuliwa na kuuwa watu 500. Ripoti kutoka nchini humo zilieleza jana jioni.

Biden alitarajiwa kukutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan, Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work At Home
Work At Home
1 month ago

Cash generating easy and fast method to work part time and earn an extra $15,000 or even more than this online. By working in my spare time I made $17990 in my previous month and I am very happy now because of this job. you can try this now by following 

the details here…… http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work At Home
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x