Biden: Urusi haiwezi kushinda vita Ukraine

Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Urusi haiwezi kushinda vita dhidi ya Ukraine.

Biden amezungumza hayo leo akiwa Mjini Warsaw nchini Poland, baada ya jana Rais wa Urusi Vladamir Putin kusema kuwa taifa lake litandeleza mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Kiongozi alifanya ziara ya kwanza Mjini Kiev, tangu uvamizi wa Urusi ulipoanza Februari 24, 2022 ikiwa ni siku chache kabla ya kutimiza mwaka mmoja madarakani .

Advertisement

Katika hotuba yake ya kila mwaka aliyoitoa jana Rais Putin aliyashutumu mataifa ya Magharibi kwa kuongeza mzozo huo na kutangaza kuwa Urusi itasimamisha ushiriki wake katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia unaojulikana kama New START ambao iliusaini na Marekani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *