UCHAMBUZI wa Takwimu uliofanywa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), umetambua bidhaa tisa za Tanzania zinahitajika katika masoko mbalimbali duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis ameeleza hayo mkoani Dar es Salaam katika taarifa yake aliyoitoa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka.
Amesema katika uchambuzi huo, Tantrade imezitambua bidhaa za dhahabu, koroho, ufuta, baazi, kahawa, dengu, almasi na vifungshio vya mifuko ndio mahitaji makuu duniani.
Amezitaja nchi ambazo zinahitaji bidhaa hizo kuwa ni India, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uswisi, Vietnam, China, Pakistani, Japani, Marekani, Oman, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia.
Amesema dhahabu mauzo halisi ni Dola milioni 2,100 lakini mahitaji katika nchi hizo ni Dola 3,400.
Vile vile mauzo halisi ya korosho ni Dola 304 lakini fursa iliyopo ni 819.
“Mauzo halisi ya ufuta ni Dola milioni 152 lakini fursa iliyopo ni Dola milioni 207,” amesema. Pia kuhusu mbaazi mauzo halisi ni Dola 95 ila fursa iliyopo ni Dola milioni 201.
Bidhaa nyingine ni kahawa ambayo mauzo halisi ni Dola 157 lakini fursa iliyopo ni Dola 171. Kuhusu dengu mauzo halisi ni Dola 64 ilhali fursa iliyopo ni Dola 154.
Amesema kuwa mamlaka hiyo inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kufikia azma ya serikali kuwa kitovu cha biashara kwa kuendeleza, kukuza na kutangaza bidhaa na huduma ndani nan je ya nchi.
Comments are closed.