Big Boss ilimnogesha Bruce Lee kwa mashabiki

KATIKA sinema hii simulizi lake limejijenga  namna ambavyo inakuwa taabu sana kutekeleza viapo vyako baada ya yule uliyemwapia kwamba hutatumia ujuzi wako wa hatari wa kupigana kudhuru watu au kujitengenezea umaarufu, kukosekana na jamaa wa karibu kuuawa.

Aidha katika kusaka wauaji unagundua kitu kingine kibaya zaidi, kwamba katika eneo lako la kazi tajiri yako anatumia ofisi hiyo katika kusambaza mihadarati na wewe ni tishio kwa kazi yake hiyo.

Katika sinema hii ndefu ambayo Bruce Lee anakuwa mnyonge sehemu kubwa ya maisha kabla hajacharuka kutokana na  mauaji ya watu wa karibu yake,ni sinema iliyomtoa sana Bruce Lee.

Advertisement

Filamu hii ya miaka ya 1970 sina uhakika kama mwenzangu ulikuwa umezaliwa, lakini ndio ukweli ilikuwa imeongozwa na  Lo Wei na ilikuwa na ndivyo ilivyo ni drama, aksheni na pia ya kutamalaki.

Ikiwa imeingia katika majumba ya sinema Aprili 1 ,1972 na kuchezwa kwa dakika 99 ni filamu ambayo sehemu nyingine kama nchini Marekani ilikosewa toleo na kuitwa Fists of Fury.

Ni picha iliyotengenezwa mwaka 1971 katika visiwa vya Hong Kong lakini bado ni tamu kama imetengenezwa jana. Bruce Lee mwenyewe alimsaidia dairekta kufanya vitu vyenye uhakika katika simulizi lake na katika aksheni.

Pamoja na Lee wengine walioshiriki ni Maria Yi, James Tien na Tony Liu.  Hii ilkikuwa ni picha ya kwanza kubwa kwa Lee na awali iliandikwa kwa ajili ya James Tien.

Filamu hii ilifanya vyema sana katika mauzo na hata wahakiki wakorofi wasiotaka Made China waliikubali.

Lee alifanya vyema katika sinema hiyo kiasi ya kwamba alimfunika mtu ambaye tayari alikuwa staa katika sinema za HongKong , mtaalamu Tien. Brucelee akawa maarufu sana katika bara la Asia kutokana na  uigizaji wake wa hali ya juu katika sinema hiyo.

Ploti zake zilikuwa tamu na fupi fupi lakini zilizosukwa vyema.Cheng Chao-an (Bruce Lee) ni Mchina mbaye anatoka kwao Uchina (bara) na kwenda Thailand kuishi na familia iliyomuasili wakati huo akiwa anataka kufanyakazi  katika kiwanda cha barafu.

Akiwa China anakutana na  binamu yake Hsu Chien (James Tien) na mdogo wake Hsu kwa bahati mbaya, wakati Hsu Chien alipoendesha tifu kutoka kwa watu waliokuwa wanajidai ubabe.

Katika tifu hili Cheng anakataa kujihusisha  kutokana na ahadi yake aliyoifanya kwa masta wake wa kutotumia mwili wake katika mapigano na ili kumkumbusha anavaa kidude katika shingo yake.

Cheng anaanza kazi katika kiwanda cha barafu. Lakini siku moja bonge la barafu moja lilipoanguka na kupasuka Cheng anagundua kwamba kumbe kati yake kuna vitu zaidi, kuna mfuko wenye unga mweupe.

Binamu wawili wa Cheng wanachukua mfuko ule na kisha wanaitwa kumuona meneja usiku ule. Kiwanda kile kumbe kilikuwa kinajihusisha na dawa za kulevya.

Bosi wa dawa hizo ni Hsiao Mi, ambaye pia alikuwa anatambuliwa kama Big Boss. Wakati binamu wale wa Cheng walipokataa kuhongwa kuficha siri waliuawa  na maiti zao kufichwa.

Hsu Chien  na binamu yake mwingine baada ya kusukuti sana wanaamua kwenda kwenye makazi ya Hsiao kuulizia nini kimetokea. Hsu anatilia shaka madai ya Hsiao kwamba hajui kimetokea nini kwa ndugu hao na kutishia kuwapeleka polisi wakiendelea kumletea vurumai nyumbani kwake.

Wawili hao wanajribu kukabiliana na genge la Hsiao Chiun na wanauawa. Wafanyakazi walipogundua kwamba hata Hsu hajulikani alipo wakanza kufanya ghasia na kuishia kukabiliana na majambazi yaliyokodiwa.

Katika vurugu zile mmoja wa wale majambazi anaking’oa kidude alichojivika Lee na katika  hamaki Lee anamtandika kisawasawa.

Kuondoa mitafaruku maneja wa kiwanda anamweka Cheng kuwa  mwangalizi na hapo jamaa zake na Cheng wakaanza kumtenga na kusema kwamba anafanya majidai. Kasoro mmoja tu ambaye hakumtenga Chaio Mei.

Katika moja ya hafla Cheng analewa na kuambatana na kahaba Sun Wu Man ambaye anamuonywa kwamba maisha yake yapo hatarini  na kwamba Hsiao Mi anaendesha uvushaji wa dawa za kulevya.

Baada ya Cheng kuondoka mtoto wa Hisiao, Hsiao Chiun, anavamia chumba cha Sun na kumuua kwa kisu. Cheng anajiingiza katika kiwanda na kukuta maiti za ndugu zake pamoja na Sun.

Akiwa pale anaonwa  na kundi la Hsaio Chiun. Cheng analazimika kupigana kujiokoa na katika vurumai lile anawaua watu wengi akiwamo Hsiao Chiun.

Anaporudi nyumbani anakuta ndugu zake wote wameuawa na Chiao Mei ametoweka.

Cheng anaenda kulia kandoni mwa mto kisha anaamua kulipiza kisasi.Hapa ndipo maksi za Lee zilipojaa.

*Imeandaliwa na Mwandishi Wetu kutoka vyanzo mbalimbali katika mtandao.

 

 

4 comments

Comments are closed.

/* */