Bil 54/- kukabili foleni Dar, Pwani

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza mameneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) nchi nzima wahakikishe hakuna foleni zitakazokwamisha na kuzorotesha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Ulega ametoa agizo hilo Dar es Salaam jana wakati akikagua maendeleo ya upanuzi wa barabara ya Mbagala Rangi Tatu – Kongowe yenye urefu wa kilometa 3.8. Aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha zaidi ya Sh bilioni 54 zitumike kwa ajili ya kutatua kero ya foleni kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
“Wakurugenzi kutoka TANROADS, ninaagiza kwa mameneja wote nchi nzima, nikisikia habari za foleni zinalalamikiwa na wananchi na hakuna suluhu ya muda mfupi na ya muda mrefu hufai kuwa Meneja,” alisema Ulega. SOMA: Mkandarasi apewa tenda ujenzi wa barabara Kagera
Aidha, Ulega ametoa angalizo kwa Mameneja hao katika kipindi hiki cha mvua zinazotarajiwa kunyesha kuhakikisha barabara hazileti athari kwa wananchi na kusababisha kushindwa kufanya shughuli zao kutokana na kukosa suluhu ya jambo hilo mapema.
“Mameneja fanyeni kazi, msikae kimazoea na kuona jambo hilo ni la kawaida, kukatika kwa barabara tafsiri yake Meneja hukagui barabara yako na kuona hapa kuna udhaifu ambao lolote likitokea pataharibika,” amesisitiza Ulega.
Vilevile, Ulega alimuagiza Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Pwani kuhakikisha anaitengeneza barabara ya zamani ya Morogoro haraka iwezekanavyo ili iweze kuwa njia mbadala ya kutatua changamoto za magari kukwama katika barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Chalinze.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Lazeck Alinanuswe ameeleza kuwa upanuzi wa barabara hiyo unatekelezwa na Mkandarasi STECOL Corporation kutoka China na kusimamiwa na Kitengo cha TECU kutoka TANROADS kwa muda wa miezi 15 na hivyo mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2026.
Mradi wa upanuzi wa barabara hiyo unahusisha upanuzi wa barabara kutoka njia mbili hadi sita, ujenzi wa Daraja la juu katika eneo la Kongowe, ujenzi wa mfumo wa maji ya mvua, njia za watembea kwa miguu kila upande, njia za pembeni kila upande na miundombinu ya usalama barabarani.




WHATSAPP ☎️+254706758878 ☎️ ZUNGUMUZA NA MIMI MGANGA MKU WAGANGA WA MITISHAMBA HAPA KENYA NA EAST AFRICA.
I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com