Bilioni 14 kuwezesha sekta ya uvuvi
Serikali imekusudia kutoa fedha Sh bilioni 14 kwa àjili ya ununuzi wa boti za uvuvi za kisasa pamoja na uwezeshaji vifaa kwa vikundi vinavyojishughulisha na kilimo cha zao la mwani.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo ya kukagua shughuli za maendeleo zilizopo kwenye sekta ya mifugo na Uvuvi.Amesema kuwa kati ya fedha hizi Sh bilioni 11.5 zitakwenda kununua boti za kisasa za uvuvi na kugaiwa Kwa vikundi vinavyojishughulisha na shughuli za Uvuvi Ili waweze kupata raslima zitokanazo na bahari Kwa wingi.
“Hizi Sh bilioni 2.5 zilizobaki zitatumika kuwawezesha wakulima wa mwani Kwa kuwa nunulia vifaa lengo ikiwa ni kuongeza uzalishaji wa mwani hapa nchini”amesema Ulega.
Mgumba amesema kuwa ili dhana ya kilimo biashara iweze kufanyakazi Kwa ufanisi inahitaji kwanza ileweke na Viongozi wa serikali kabla ya kwenda Kwa wananchi.
“Sekta ya kilimo Kwa kiwango kikubwa imesimamiwa na sekta binafsi hivyo Ili kuhakikisha inakuwa na tija inayokusudiwa lazima Viongozi tujue kilimo biashara kinataka nini “amesema RC Mgumba