DAR ES SALAAM: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali imeendelea kuithamini sekta ya afya kwa kutenga bajeti itakayopunguza changamoto mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano JNICC Dar es Salaam leo, Oktoba 28, 2023, Waziri Ummy amesema kiasi cha Shilingi bilioni 20 kununua dawa kila mwezi.
Ameongeza kuwa licha ya fedha nyingi kuelekezwa katika miundombinu ya afya, serikali pia imekuwa ikipambana na upungufu wa dawa katika vituo vya afya na ndio maana bejeti katika huduma hiyo inaongezeka kila wakati.
Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mgeni rasmi katika tukio hilo.