Sh bilioni 52 zatumika ujenzi shule za msingi, sekondari Mtwara

SERIKALI imetoa kiasi cha Sh bilioni 52.8 kwa Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule za msingi na sekondari mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema fedha hizo zilitolewa kuanzia Julai 2021 mpaka Juni 2023.

Kanali Abbas ametoa taarifa hiyo leo tarehe Julai 11, 2023 wakati akikabidhi magari matatu kwa wakurungezi watendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na Nanyamba mji kwa ajili ya shughuli ya ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za sekondari.

Amesema fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa shule mpya za sekondari 10 kwa mwaka 2021/2022 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 4.7 zilitumika.

Sh milioni 950 zilitumika ujenzi wa nyumba za walimu 10 katika shule za sekondari 10 kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

Sh bilioni 3.7 zilitumika katika ujenzi shule mpya 10 za msingi kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

Kiasi cha Sh bilioni 3 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa inayojengwa Wilaya ya Nanyumbu.

Ujenzi wa mabweni 20 , madarasa 45 na vyoo matundu 77 katika shule za sekondari kwa ajili hakupokea wanafunzi wa kidato cha tano 2022/2023 ambapo kiasi cha Sh bilioni 3.8 zilitumika.

Ujenzi wa vyuo vya VETA Tandahimba na Nanyumbu kwa shilingi bilioni 2.8.

Kanali Abbas amewata wakuu wa Wilaya kuhakikisha mamlaka za serikali zinatumia magari yaliyotolewa na serikali kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji shuleni huku akisisitiza magari yasipangiwe shughuli nyingine.

“Ninaomba nitumie fursa hii kumwelekeza Katibu Tawala wa Mkoa kusimamia utekelezaji wa maelezo hayo ya serikali,” amesema.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button