SERIKALI imetoa Sh bilioni 9.8 kutekeleza miradi saba ya maji katika Wilaya za Mtwara na Tandahimba mkoani Mtwara.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mtwara, Primi Damas ametoa taarifa hiyo leo katika hafla ya kusaini mikataba ya utekelezaji wa miradi hiyo kati ya wakala huo na wakandarasi.
Amesema utekelezaji wa miradi hiyo itanufaisha wakazi 67,149 wa vijiji 35.
“Kukamilika kwa miradi hii utaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 17 Wilaya ya Tandahimba na asilimia 5.
8 kwa Wilaya ya Mtwara,” amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas ameishukuru serikali na kuwataka viongozi wilaya hizo kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ubora unaoendana thamani ya pesa iliyotolewa.
“Miradi ni mikubwa , viongozi simamieni ili ukamilikaje wake utatua changamoto ya maji kwa mkoa wetu.” Amesema RC Abbas.
Pia amewataka wakandarasi waliosaini mikataba ya utekelezaji kwenda eneo la kazi, kuanza kazi na kuhakikisha miradi inakamilika ndani au kabla ya muda uliowekwa kwenye mikataba. Mikata yote saba inatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.