Bima ya afya haiepukiki – Rais Samia
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ili kuendelea kutoa huduma za afya endelevu suala la bima ya afya kwa kila mtu haliepukiki.
Rais Samia ameyasema hayo leo Januari 10, 2024 katika ufunguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi (Lumumba)
Amesema, hospitali hiyo ya Lumumba itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa na kutoa huduma bora zinazokusudiwa.
“Suala la bima ya afya haliepukiki tujipange kila mmoja kuwa na bima ili tutibiwe vile ipasavyo,” amesema.
Pia ameeleza kufarijika kuwepo kwa wataalamu katika hospitali hiyo, na kutoa rai kwa Wizara ya Afya kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.