Bima ya malengo mkombozi,

watanzania watakiwa kujidundulizia

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limewataka watanzania kujiwekea bima ya malengo ili kuandaa kesho yao na familia zao.

Akizungumza na HabariLeo leo Julai 2, 2023 Afisa Bima, Upendo Shengena amesema kuwa bima ya malengo ni mkombozi kwa watanzania ambapo itamsaidia kufikia malengo yake.

Amesema bima hiyo ya malengo ni kuanzia miaka 10 ambapo mbima ataanza kunufaika kwa kupata faida ya asilimia 5.5  baada ya miaka miwili tangu kuanza kuchangia.

Akifafanua zaidi kuhusu bima hiyo ya malengo,  Afisa Tehama wa NIC, Abdulhafidh Kibiki amesema mbima atapata asilimia hiyo ya 5.

5 ya kiwango alichochangia kulingana na thamani ya bima,

“Baada ya miaka miwili ya uchangiaji, mbima atakuwa akipata faida hiyo kila mwaka, na mwisho wa bima unapata thamani ya bima ambayo ni pesa yako yote pamoja na faida ambazo ulikuwa unarudishiwa kila mwaka.”Amesema na kuongeza

“Pia, ikitokea bahati mbaya mbima akapatwa na umauti wale tegemezi watapata ile pesa yote ambayo alitegemea kupata yule aliyekata bima angepata baada ya miaka 10.”Amesema

Amefafanua kuwa kama bima ina thamani ya sh milioni 100 ikatokea amechangia mwezi mmoja akafariki basi wategemezi wake watapata kiasi chote cha fedha ambazo angekipata mbima ndani ya miaka 10.

“Kiwango cha bima kinatokana na uwezo wako, mbima ndio anapanga malengo yake kuna wengine wanataka baada ya miaka 10 apate milioni 100, wengine milioni 50 wengine milioni 20 sasa hapo  unaangalia uwezo wako ili utimize malengo yako.”Amesisitiza.

Habari Zifananazo

Back to top button