Bingwa wa leo kuvuna Dola milioni 42

Mshindi wa fainali leo ya Kombe la Dunia, kati ya Argentina na Ufaransa, ataondoka na Dola milioni 42 sawa na Shilingi bilioni 98.319.

Atakayemaliza nafasi ya pili atavuna dola milioni 30 sawa na Shilingi bilioni 70 huku.

Baada ya kushika nafasi ya nne katika mashindano ya Kombe la Dunia, timu ya Taifa ya Morocco imevuna Dola milioni 25 ambazo sawa na Shilingi bilioni 58.523.

Morocco imeshika nafasi hiyo baada ya kufungwa na Croatia mabao 2-1 na mpinzani wake kushika nafasi ya tatu hivyo kuondoka na Dola milioni 27 sawa na Shilingi bilioni 63.

Timu nne zilizofuzu robo-fainali wote watapata Dola milioni 17 sawa na Shilingi bilioni 39 timu nane zilizoshindwa katika hatua ya 16 bora zikiondoka na Dola bilioni 13 sawa na Shilingi bilioni 30.

Mataifa mengine 16 ambayo yalitolewa katika hatua ya makundi yanapewa Dola milioni tisa, ambazo sawa na Shilingi bilioni 20 bila kujali ni pointi ngapi walizopata katika michezo yao mitatu.

Kila taifa linapaswa kuamua ni kiasi gani cha fedha hizo wanachotoa kwa wachezaji na wafanyakazi. Huo huwa ni uamuzi unaofanywa kabla ya michuano hiyo huku malengo ya utendaji yakiwa yamepangwa kwa ushindi katika kila hatua ya Kombe la Dunia.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button