Bingwa wa singeli kuzawadiwa gari

DAR ES SALAAM; MKURUGENZI wa Efm Redio, Francis Ciza maarufu kwa jina la Dj Majizzo  ameweka zawadi ya gari kwa msanii bora wa muziki wa singeli nchini.

Dj Majizzo amesema suala hilo lilianza kama utani, lakini sasa ameamua kutoa gari hilo lenye thamani kubwa, ili kuondoa utata wa nani bingwa halisi wa muziki huo nchini baada ya wasanii hao kila mmoja kujiona bora kuliko wenzake.

“Tumekuwa na wasanii wengi wa muziki wa singeli, lakini hatujui nani mkali kuliko wenzake, hivyo naweka Mercedes-Benz lishindaniwe na tupate mkali wa singeli Tanzania na hii italeta heshima kubwa kwa wasanii wa singeli ndani na nje ya nchi,” amefafanua Dj Majizzo.

Amesema wasanii watakaoshindanishwa watachujwa na kufikia watano hatua ya fainali, ambapo shindano hilo litaanzia ngazi ya mtaa, studio na fainali yake itafanyika ukumbi wa Mlimani City.

 

Habari Zifananazo

Back to top button