Biteko aagiza Ofisa uhusiano TPDC kuondolewa

MTWARA; NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko amemuagiza Mkurungenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kumuondoa mara moja kazini Ofisa Uhusiano  wa shirika hilo na kuweka mtu mwingine kwa kushindwa kufanya kazi yake.

pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (tanesco), kumsimamisha kazi Meneja wa Huduma kwa wateja kwenye shirika hilo na kuweka mtu mwingine kufanya hiyo kazi.

Biteko ametoa maagizo hayo  leo Novemba 14, 2023, wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Msimbati, Halmashauri ya Mtwara, mkoani Mtwara.

Advertisement

Kwa upande wa Ofisa Uhusiano TPDC, Biteko amesema ameshindwa kufanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa , kusikiliza kero kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya miradi ya gesi nchini. Ofisa Uhusiano TPDC, Biteko amesema ameshindwa kufanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa , kusikiliza kero kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya miradi ya gesi nchini.

Kuhusu Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanesco,  amesema amekuwa akitoa majibu yasiyoridhisha kwa wateja pindi wanapopiga simu kwenye shirika kupata majibu kutokana na tatizo la umeme.

“Tanesco tuna kitengo cha huduma kwa mteja , ni kweli tuna changamto ya umeme, lakini watu wakipiga simu majibu wanayojibiwa wananiandikia meseji, wanalalamika wakisema majibu tunayopewa waziri sio yenyewe,” amesema.

Biteko ambaye alioneshwa kukerwa na mwenendo wa meneja huyo wa huduma kwa wateja amesema ni lazima watendaji serikalini wawajibike ipasavyo.

“Nimemuelekeza Mkurugenzi wa Tanesco yule Meneja wa huduma kwa wateja pale Tanesco ondoa mara moja, weka mtu mwingine,” amesema na kuongeza

“Lazima tuheshimiane kazi ifanyaike, wananchi wanataka umeme, watu wanataka gesi, watu wanataka gesi ibadilishe maisha yao, hatuwezi kuja hapa tumevaa tumependeza watu wanalia shida ndogo ndogo,” amesema.

 

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *