Biteko atoa maagizo makali kwa EWURA

DODOMA: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dk. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuzingatia maslahi ya Watanzania na maslahi ya nchi katika kazi zao za Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ili Watanzania wapate huduma bora na kwa unafuu mkubwa.

Dk. Biteko amesema hayo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa mamlaka hiyo kilichofanyika  Novemba 8, 2023 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Rugemalira Rutatinwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,  Ziana Mlawa.

“Tambueni kuwa taifa lina mategemeno makubwa na ninyi, hivyo fanyeni kazi zenu kwa weledi na ubunifu mkubwa unaoendana na kasi ya teknolojia na maendeleo ya dunia; kanuni na miongozo yenu mnayotumia katika utekelezaji wa majukumu iundwe katika mifumo rafiki kulingana na hali iliyopo ili ilenge kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa na hivyo Watanzania waendelee kupata huduma bora na kwa gharama stahiki.” Amesema Dk. Biteko

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mkuu ameipongeza EWURA kwa kupitia upya gharama za uagizaji wa mafuta ambazo amesema kuwa, awali zilikuwa kubwa na zilikuwa zikipelekea athari mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa gharama katika Sekta ya Usafirishaji na Uzalishaji.

“Gharama hizi za uagizaji mafuta zilikuwa kubwa mno huku kukiwa hakuna sababu ya kuwa kubwa kwa kiasi hicho, niliwapa maelekezo mkazitazame upya, nashukuru mmeziangalia na ninafurahi kwamba zimeshuka na hivyo kupunguza makali kwa watumiaji.” Amesema Dk. Biteko.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile alisema kuwa, Taasisi hiyo imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi lengo likiwa ni kuhakikisha huduma za nishati na maji zinapatikana kwa uhakika, kwa kutosha, kwa uendelevu na kwa gharama ambazo wananchi wanazidumu.

Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA kinachoendelea jijini Dodoma kimelenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa bajeti ya EWURA kwa mwaka 2022/2023 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu za EWURA za mwaka 2022/23.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Marie Allen
Marie Allen
24 days ago

I get paid more than $140 to $170 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily $25k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
.
.
.
Here is I started.…………>> http://Www.Smartcareer1.com

Julia
Julia
24 days ago

Everybody can earn 500 dollars daily. Yes! you can earn more than you think by working online from home. I have been doing this job for like a few weeks and my last week payment was exactly 30,000 dollars.
.
.
Detail Here—————————————————————>>> http://Www.BizWork1.Com

Eileenritchett
Eileenritchett
24 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 24 days ago by Eileenritchett
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x