BAADA ya Simba kupangwa Kundi C, kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Nahodha wa miamba hiyo ya soka nchini John Bocco leo Desemba 14, amewataka wachezaji wenzake kucheza kwa kujituma zaidi na siyo kujivunia rekodi zao za mashindano yaliyopita.
Akizungumza na SpotiLeo, mchezaji huyo ameeleza kuwa kucheza kwa mazoea kunaweza kuwavurugia mipango yao na kushindwa kufikia malengo hivyo nilazima wacheze kwa kujituma bila kudharau timu yoyote waliyopangwa nayo
“Kwenye kundi letu kuna Vipers wengi wanaidharau kwakua ni timu ngeni kwenye hatua hiyo lakini hii siyo timu ya kuibeza mpaka imefika hapo imezitoa timu kubwa Afrika kwahiyo ili tuweze kufikia malengo yetu lazima tucheze mechi hizi za makundi kwa kujitoa na kujituma bila kuangalia kuwa tunauzoefu kiasi gani, amesema Bocco.
Mshambuliaji huyo ameeleza kuwa pia ameitaja Raja Casablanca kuwa ni miongoni mwa timu nzuri kwenye kundi lao hivyo kwake ni kundi gumu na wanapaswa kupambana kuonesha ukumbwa wao katika mashindano hayo
Bocco amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwapa sapoti kwenye mechi zao za nyumbani ili waweze kuchukua pointi zote tisa
Comments are closed.