Bodaboda waonywa uvunjifu wa sheria
MKUU wa Dawati la Elimu ya Usalama Tanzani TRAFIC ACP Michael Delali amewataka wanaosafirisha abiria kwa chombo cha pikipiki (Bodaboda) kutii sheria ikiwemo ya uvaaji kofia ngumu na kuacha tabia ya kubeba abiria zaidi ya mmoja ili kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za pikipiki .
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Kampeni ” vaa kofia achana na mshiko ” mafunzo ya bodaboda yatakayotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali Tunaweza Forum itakayoendeshwa 2023/2024 ndani ya miezi 10 katika wilaya ya Kinondoni, Temeke, Ubungo , Ilala, na Kigamboni.
Amesema taasisi hiyo wameweza kushirikiana na wadau mbalimbali ili kusaidia kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto maarufu kama bodaboda ili kusaidia kupunguza tatizo la kutovaa kofia ngumu wakati anatumia chombo cha moto hata ajali ikitokea kupona ni bahati nasibu .
“Sheria ya usalama barabarani iko kwa ajili ya kunusuru ajali lakini imekuwa ikivunjwa utakuta kuna mtindo bodaboda hajavaa kofia abiria hajavaa kofia mwendo mkali alafu dereva mwenyewe pia kavaa ndala ikitokea breki ikifeli Kisigino cha mguu ndiyo kitageuzwa. breki na barabara zetu kokoto lazima ajali itokee hivyo abiria kabla ya kupanda pikipiki mkagua dereva wako na akuvalishe kofia ngumu. ” amesema ACP.
Mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tunaweza Forum, Zabron Kamoga amesema katika kampeni yao watakwenda na fursa mbalimbali kwa bodaboda ikiwemo wataalamu kuwafundisha kuweka. akiba kwa maisha ya baadae, kufungu akaunt. ya NMB kuomba mikopo, kuwekeza kwa UTT AMIS NSSF.