Bodi Simba SC yateua wenyeviti wa kamati mbalimbali

BODI ya Wakurugenzi ya Simba SC imefanya uteuzi wa nafasi ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wake katika kamati mbalimbali za klabu hiyo.
Katika taarifa yao, Simba imeeleza kuwa uteuzi huo umezingatia ibara ya 33 (5) 37 ya katiba yao ya mwaka 2018.
Kamati ya Maadili, Mwenyekiti ni Charles Kanyela, na makamu mwenyekiti wake ni Anne Mareale. katika kamati hiyo wajumbe ni Saleh Pamba, Jasper Monyo na Saleh Mwachaka.
Aidha, katika kamati ya nidhamu, Mwenyekiti ni Suleiman Kova, makamu wake ni Samson Mbamba, wajumbe wa kamati hiyo ni Mohammed Ally, Hassan Hassanoo na Peter Mwitwa. Simba imeeleza kuwa wateuliwa hao wataanza kazi mara baada ya uteuzi huo.