Bodi ya wahasibu yatangaza ufaulu

JUMLA ya watahiniwa 4,205 kati ya watahiniwa 6,837 waliosajiliwa katika vituo 12 nchini wamefaulu mitihani ya 97 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA).

Kati ya watahiniwa 6,837 waliosajiliwa waliofanya mitihani walikuwa ni 6,332 sawa na asilimia 92.6 huku 505 hawakuweza kufanya mitihani.

Watahiniwa hao 4,205 sawa na asilimi 66.

4 wamefaulu mitihani yao ambapo kati yao watahiniwa 134 wamefaulu ngazi husika katika mkao mmoja wengine 53 wamefaulu masomo waliyokuwa wameshindwa mihula ya awali.

Akitoa matokeo Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof Sylvia Temu amesema kwa ngazi ya Shahada ya Juu ya Uhasibu (CPA) jumla ya watahiniwa 394 wamefaulu ambapo hii inafanya watahiniwa waliofaulu mitihani ya CPA kufikia 12,547 tangu kuanza kwa mitihani hiyo mwaka 1975.

“Mitihani ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza nay a pili katika ngazi ya cheti cha Utunzaji wa Hesabu (ATEC 1,ATEC II) zenye masomo manne kila mmoja ,Ngazi ya Taaluma hatua ya msingi(Foundation Level) yenye msomo sita ,hatua ya kati yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne,”ameeleza Prof Temu.

Habari Zifananazo

Back to top button