Bomba la mafuta laleta neema

ZAIDI ya Watanzania 3619 pamoja na kampuni ya kizawa 50, wamenufaika na fursa ya ajira pamoja na huduma mbalimbali katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kwa kipindi cha mwaka mmoja wa utekelezaji wake.

Takwimu hizo  zimetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia wanawake na makundi maalum Dk Dorothy GwajiMa kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati wa kongamano la wanawake na manunuzi ya umma linalofanya jijini Tanga.

Advertisement

Amesema kuwa katika eneo la utekelezaji wa ujenzi ya mradi huo jumla ya vijana 120 wa kitanzania wamepata mafunzo ya amani kwa ajili ya kushiriki kwenye ujenzi huo katika viwango vya kimataifa.

“Niwaombe Watanzania mnapotekeleza miradi hii ya kimkakati na yenye tija kwa Taifa letu kuifanya kwa nidhamu, weledi na uwadilifu mkubwa, ili kuendelea kutangaza sifa njema za Taifa hili,” amesema Waziri Gwajima.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya ufuatiliaji na tathimini ya ushiriki wa wanawake na makundi mengine, ili kubaini kama kuna  changamoto katika ushiriki wa wananchi wazawa na kuzichukulia hatua stahiki kwa haraka.

4 comments

Comments are closed.