Bosi Fifa atishia kujiuzulu kisa ‘pombe’ Qatar 2022

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema kama pombe ndilo suala kubwa linalopigiwa kelele kuelekea Kombe la Dunia basi atajiuzulu mara moja na kwenda ufukweni kupumzika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nchini Qatar, Infatino amesema kutokuwepo kwa pombe viwanjani kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza kesho huko Qatar ni jambo jema tu.

“Usipokunywa bia kwa masaa mawili matatu, unaweza kuishi kuna nchi nyingi zinapiga vita pombe viwanjani ikiwemo Ufaransa.”amesema Infantino.

Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali ya Qatar kupiga marufuku uuzaji wa vinywaji hivyo maeneo yanayozunguka viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo

Infantino amesema kuwa nchi za Magharibi zisiikosoe Qatar kwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia, na badala yake nchi hizo zinatakiwa kuiomba radhi nchi hiyo kwa historia zao.

Taarifa ya mtandao wa Skysport imeeleza kuwa, Infantino amesema hakuna mkosoaji yoyoye kati yao anayeweza kufundisha watu maadili. hatua hiyo ni kutokana na vikwazo vinavyotokana na sheria za nchi hiyo vilivyowekwa kwa wageni kuelekea mashindano hayo.

Infantino alisema: “Tumefundishwa masomo mengi kutoka kwa Wazungu na ulimwengu wa Magharibi. Mimi ni Mzungu. Kwa kile ambacho tumekuwa tukifanya kwa miaka 3,000 duniani kote, tunapaswa kuomba msamaha kwa miaka 3,000 ijayo kabla ya kutoa masomo ya maadili.


“Nina ugumu wa kuelewa ukosoaji, tunapaswa kuwekeza katika kuwasaidia watu hawa, katika elimu na kuwapa maisha bora ya baadaye na matumaini zaidi. Sote tunapaswa kujielimisha, mambo mengi sio kamili lakini mageuzi na mabadiliko huchukua muda.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x