BOT: njooni mjisajili muhula mpya wa masomo

USAJILI wa mwaka mpya wa masomo katika Chuo cha Benki Kuu (BOT) unafanyika katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayoendelea ambapo BOT inashiriki katika maonesho hayo.

Akizungumza na HabariLeo, Mratibu wa Mafunzo wa chuo cha BOT, Tulla Mwigune amesema chuo hicho kimekua kikitoa kozi mbali mbali za kifedha kwa wanafunzi wa kidato cha nne, sita na kuendelea.

Anasema tangu mwaka 2020 chuo hicho kimeanza kutoa kozi za kuwajenga vijana kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita, kozi hiyo inaitwa ‘Odinary Diploma’ inatolewa kwa miaka miwili.

Amesema vigezo vya kujiunga ni kwamba mwanafunzi awe amefaulu masomo mawili  yaliyobalansi na ada yake ni sh milioni 1.350  na inalipwa kwa awamu mbili.

“Lakini kuna wale waliohitimu kidato cha nne, tunawapokea lakini wawe wamesoma masomo ya Biashara au Afisa Rasilimali Watu au Mahesabu katika chuo ambacho kinatambuliwa na serikali,”amesema Tulla.

Aidha, amesema piia kuna programu ya ‘post graduate diploma and bank management’ imeandaliwa mahususi kwa watu ambao wamemaliza ‘degree’ ya kwanza lakini wanataka kujiendeleza kwenye masuala ya kibenki au biashara kwa ujumla wanaweza kujiunga.

“Program hii inatolewa hapa hapa Dar kwa miezi tisa, ada yake ni Sh milini 2.5 na inalipwa kwa awamu tatu.”Amesema

Habari Zifananazo

Back to top button