BoT yaja na muongozo mikopo kausha damu

DAR ES SALAAM :BENKU Kuu ya Tanzania (BoT), imesema ipo mbioni kutoa miongozo na kanuni mpya kwa ajili ya kuratibu na kutoa huduma ndogo za kifedha daraja la pili, ili kukabilina na changamoto zilizopo ikiwemo uvinjifu wa utu, sheria na maadili katika utoaji mikopo.

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma za ndogo za kifedha daraja la pili, Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, amesema kumekuwepo na malalamiko mengi kutokana na vitendo vya ukiukaji maadili na utu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma ndogo za kifedha, hali inayoharibu biashara ya sekta ya fedha.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo BoT, imeamua kuja na miongozo na kanuni zitakazosaidia kurekebisha sekta ya fedha hasa katika mikopo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msimamizi wa Fedha BoT, Sadat Mussa, amesema licha ya mafunzo hayo tayari wameshafanya uelimishaji kwa watoa huduma zaidi ya 1,000 nchi nzima, licha ya kuwa wameamua kufanya
mafunzo mafupi kwa watoa huduma ndogo za kifedha, ili kupunguza ama kuondoa kabisha changamoto zilizopo.

Nao baadhi ya watoa huduma ndogo za kifedha, Julieth Charles na Tilda Kinaro wamesema sasa ni kweli kuna baadhi yao wamekuwa wakikiuka sheria na taratibu, hivyo ni muhimu kupatiwa mafunzo hayo, huku wakiwataka wananchi pia kuheshimu na kupata elimu ya mikopo, ili kuondoa lawama .

Habari Zifananazo

Back to top button