BOT yawaita watanzania kununua hatifungani

Yawataka wasiogope kima cha chini Sh milioni 1

BENKI Kuu ya Tanzania BOT imewataka watanzania wa ndani na waishio nje ya nchi ‘diaspora’ kuja kuwekeza kwenye dhamana (hati fungani) za serikali kwani ni salama kwa fedha zao

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 10, 2023 katika banda la BOT lililopo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba 2023’ na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha BOT, Ephraim Madembwe.

Amesema,  Watanzania wasione hati fungani kuwa ni kwa matajiri tu, mtu yoyote anaweza kuweka, kima cha chini ni sh milioni 1, hivyo  Mtanzania yeyote anayo fursa ya kuwekeza.

“Mtanzania yeyote anaweza kuja  kuwekeza kwenye zamana za serikali kuanzia wale wenye mtaji wa sh milioni moja hadi wenye vipato vikubwa zaidi.”Amesema Madembwe..

Amesema Serikali mwaka jana mwezi wa tano ilibadilisha sheria ambayo mwanzoni ilipunguza wigo wa kuuza wakazi wanaoishi nje ya Tanzania lakini baada ya sheria kubadilishi wakaazi wote ambao wanaishi nchi za SADC  na hata waliopo nje wanaruhusiwa kuwekeza, na dhamana hizi tunawalenga hasa ‘Daispora’

Amesema faida ya kuwekeza kwenye dhamana za serikali ni  fursa kwa kuwa ukiwekeza kwenye dhamana za serikali, hawatakuwa na hatari ya kupoteza, uwekezaji wowote unaadhiriwa pale unapopoteza.

“Pia ukiwekeza kwenye dhamana za serikali una uwezo wa  kutumia dhamana yako kupata mkopo, inakuwa kinga ya mkopo.”Amesema

Aidha, amesisitiza “Uwekezaji wa dhamana za serikali, kwa ambao hawafahamu ipo fursa ya kuwekeza, zamana za serikali ni nyezo ambayo serikali inatumia kukopa kwenye soko lake la ndani.

Akifafanua amesema, kwa mwaka huu wa  fedha huu 2023, 2024 serikali imepanga kutumia Sh trilioni 44.4 sasa kwenye eneo hilo ambalo serikali kupitia wabunge wameshapitisha, serikali ni lazima itafute rasilimali fedha.

“Eneo moja wapo ambayo serikali inatafuta fedha ni kwa kuuza dhamana za serikali kwa hiyo kwenye maonesho haya tunawambia kuhusu hizi fursa na umuhimu wa kuwekeza.”Amesema.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button