Bournemouth yaiduwaza Liverpool

LIVERPOOL imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bournmouth katika mchezo wa kwanza wa EPL ulioisha hivi punde Uwanja wa Vitality.

Bao pekee la “The Cherries” limefungwa na Philip Billing dakika ya 28 kipindi cha kwanza.

Kipigo hicho kinaifanya ‘The Reds’ kubaki na pointi 42 hivyo kushindwa kupanda mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England ‘EPL’.

Advertisement

Kwa upande wa Bournemouth wamesogea mpaka nafasi ya 16 na kutoka mkiani ukiwa ni ushindi wao wa sita msimu huu ikiwa imecheza michezo 26 ya ligi hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *