Maombolezo siku tatu Brazil kifo cha Pele

Taifa la Brazil limeanza maombolezo ya siku tatu kufuatia kifo cha nguli wa soka Pele.

Pele (82) alifariki dunia jana kwa ugonjwa wa saratani. Amewahi kushinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa na timu ya Taifa ya Brazil.

Shughuli ya kumuenzi itafanyika Jumatatu ijayo kwa saa 24 katikati ya uwanja wa Santos, ambako ndiyo klabu ya Pele ya nyumbani ambapo alianza kucheza soka.

Advertisement

Jumanne kutakuwa na Gwaride, gari maalumu itakayokuwa imebeba jeneza lake litazunguka jirani na mahali ambapo mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 100 anaishi, baada ya hapo kutakuwa na maziko ambayo yatahudhuriwa na watu wachache sana.

Wanasoka, wanasiasa mashuhuri na wanaburudani kutoka pande mbalimbali za dunia wameendelea kutuma salamu zao za heshima na rambirambi kufuatia kifo cha nguli huyo wa soka.

1 comments

Comments are closed.