#BREAKING: Mlipuko watokea nje ya Wizara Afghanstan
Mlipuko mkubwa umetokea muda mchache uliopita nje ya Wizara ya Mambo ya Nje katika Mji Mkuu wa Kabul nchini Afghanstan.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa mlipuko huo umesababisha vifo ambavyo idadi haijulikana.
“Mlipuko huo umetokea mchana huu 4pm (1130 GMT)” .
Msemaji wa jeshi la polisi, Khalid Zadran amesema. Ameongeza kuwa “timu ya usalama imefika eneo la tukio.
”ameongeza Zadran.
Kwa mujibu wa taarifa ya Al-Jazeera, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Taliban hajazungumzia wala kusema chochote kuhusu tukio hilo.