Brighton yaikatili Chelsea

PAUNI milioni 80 iliyotolewa na Chelsea kwa ajili ya kumnasa Moise Caicedo imekataliwa na Brighton & Hove Albion.

Brighton wanadaiwa kukataa ofa hiyo kwa mara ya pili na inasemekana wamepanga kumbakisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador.

Caicedo ameonekana akiwa kwenye uzinduzi wa jezi mpya, ambapo leo atakuwa kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Newcastle United.

Bosi wa Brighton De Zerbi wiki iliyopita alisema anapanga kuwa na Caicedo kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Mchezaji huyo alikuwa kiungo muhimu katika kikosi kilichomaliza katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu msimu uliopita, na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Europa.

Caicedo aliomba kuondoka Brighton mwezi Januari huku Arsenal ikiwa na nia ya kumsajili.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button