Buffon astaafu soka
BREAKING: Goli kipa mkongwe raia wa Italia, Gianluigi Buffon amestaafu soka, kwa mujibu wa Fabrizio Romano Buffon atatangaza rasmi siku chache zijazo.
Buffon, 45, alikuwa akiitumikia Parma msimu uliopita.
Muitaliano huyo alianza kuitumia klabu ya Parma mwaka 1995, ambapo mwaka 2001 aliachana na timu hiyo na kujiunga na Juventus zote za nchini Italia.
Mwaka 2018 aliondoka na kujiunga na Paris Saint Germain, alidumu hapo kwa msimu mmoja na mwaka 2019 akarejea Juventus, baada ya kucheza mechi 17, mbele ya kipa Wojciech Szczęsny mwaka 2021 akajiunga na Parma.
Mafanikio makubwa ambayo Buffon ameyapata katika maisha yake ya soka ni kushinda Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na Taifa la Italia, baada ya kuwafunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalti.
Lakini pia amewahi kushinda taji la Ligi Kuu Italia maarufu ‘Seria A’ mara 10, na kuchukuwa tuzo ya kipa bora mara 13 wa ligi hiyo.
Buffon aliwahi kushinda tuzo ya kipa bora wa UEFA na mchezaji bora ngazi ya klabu mwaka 2002/2023.
Amewahi pia kuchukua tuzo ya kipa bora Ulaya mwaka 2003, 2016, 2017. Lakini pia kipa bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2016/2017.
Akiwa na PSG amewahi kushinda ubingwa wa Ligue 1 mwaka 2018/2019.