Bugando, GPITG kuboresha huduma za afya kieletroniki

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando iliyopo jijini Mwanza kwa mara nyingine imeingia mkataba na Kampuni ya Utengenezaji wa Mifumo ya Kielektroniki Sekta ya Afya (GPITG) kwa lengo la kuendelea kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma za afya hospitalini hapo.

Akizungumza leo Januari 11, 2024 jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Fabian Massaga amesema mfumo wa utoaji huduma wa ‘eHMS’ unaotumiwa na kampuni hiyo umekuwa ukitumika kwa muda mrefu hospitalini hapo, hivyo wameona umuhimu wa kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo.

“Mfumo huu Sisi kama taasisi ni mfumo mzuri na bora ambao kwakweli umetusaidia katika kuendesha shughuli zetu za kila siku.” Amesema Massaga.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa GPITG, Adelard Kiliba amesema licha ya kuaminiwa na kufanya kazi na hospitali hiyo, lakini pia wamekuwa wakihudumia hospitali tofauti ikiwemo za Serikali na binafsi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo, mkurugenzi huyo amefafanua kuwa nia yao ni kuona jinsi gani mifumo hiyo inaweza kutoka huduma, kuboresha na kuongeza ufanisi katika sekta ya afya.

Ameeleza kuwa utengenezaji wa mifumo hiyo imezingatia vigezo vyote ya Serikali ikiwemo bima, idara ya afya na serikali mtandao.

“Watoa huduma wanakuwa na mazingira bora ya ufanyaji kazi mfumo unaweza kutumika katika hospitali kubwa kama Bungando hata nje ya Tanzania.”

Kwa mujibu wa Fabian Massaga, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando hospitali hiyo na Kampuni ya GPITG zimeanza kufanya kazi tangu mwaka 2017.

Habari Zifananazo

Back to top button