Bukoba waipongeza Tarura ujenzi wa barabara

KAGERA; Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba, limeipongeza serikali kwa kuongeza bajeti ya utekelezaji wa miradi ya barabara za mjini zinazotekelezwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini ( TARURA).

Meya wa Manispaa ya Bukoba, Gibson Godson akifungua kikao cha utekelezaji wa robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 aliungana na madiwani wengine kutoa pongezi kwa Tarura.

Advertisement

“Tutoe shukrani za kipekee kwa Tarura, hakuna kero ya kujaa kwa maji , miundombinu ya barabara iko imara na vijana wanachapa kazi,hata wale wanaotaka kusafirisha bidhaa na kufanyashughuli zao mpaka usiku hawapati ugumu tena.

“Hivyo vitendo vya kupata madhara  katika barabara zisizo rasmi vimeisha na sasa ni wananchi kuimarisha uchumi wao kupitia barabara zilizotengenezwa na serikali,”amesema Godson

Meneja wa TARURA Manispaa ya Bukoba, Mhandisi Kenneth Dushime, amesema ndani ya robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024, tayari barabara za  kiwango cha lami zinaendelea kukamilishwa, ikiwemo barabara ya Ihungo.

 

Amewahakikishia madiwani wa Manispaa ya Bukoba kuwa miradi ya barabara inayotekelezwa, itaendelea kutoa ajira kwa wakandarasi wazawa na kutoa ajira kwa vijana wanaoishi katika eneo la mradi, ili kuendelea kukuza uchumi wa maeno yao.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *