MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amewashauri Watanzania kufuata utaratibu wa kununua ardhi ili kuepuka migogoro inayotokana na baadhi ya wamiliki kuuza viwanja kwa wateja zaidi ya mmoja.
Akizungumza katika mahojiano maalumu leo Machi 23,2023 na mkuu wa kitengo cha mitandao ya HabariLeo, DailyNews na SpotiLeo, Sylvester Domasa, Bulembo amesema wananchi wanapaswa kununua viwanja kutoka halmashauri, kwani migogoro mingi inatokea kwa wanaonunua ardhi ni baina ya mtu na mtu.
“Wengi ambao wanakuja katika ofisi zetu tunawapa ushirikiano, malalamiko hayakuwa hayapo kabisa”.
amesema Bulemo, DC Kigamboni.
Bulembo amefafanua kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wenyeviti na watendaji wa mtaa na wananchi pia, namna nzuri ya kununua ardhi ili kuepuka migogoro hiyo.