Bunge la China limemkabidhi Xi Jinping mwenye umri wa miaka 69 muhula wa tatu wa kihistoria kama Rais; imemchagua tena kama mkuu wa Tume Kuu ya Kijeshi kwa kura ya kauli moja ya ‘ndiyo’.
Wajumbe 3,000 wa Bunge la Kitaifa la Wananchi (NPC), bunge la China walimpigia kura kwa kauli moja Xi baada ya katiba kubadilishwa ili kuondoa ukomo wa jadi wa mihula miwili ya wadhifa huo.
Chama cha NPC, ambacho wanachama wake wameteuliwa na chama tawala cha Kikomunisti, kilimpigia Xi kura 2,952 kwa takriban saa moja. Xi pia aliteuliwa kwa kauli moja kuwa kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Watu milioni mbili.
Nguvu ya Xi inatokana na yeye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti na Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi (CMC). Alikabidhiwa nyadhifa zote mbili katika kongamano la chama Oktoba mwaka jana.
Kuthibitishwa kwa muhula wake wa tatu kama rais kulitarajiwa na wengi. Kutajwa kwa waziri mkuu mpya na mawaziri mbalimbali katika siku zijazo kunachukuliwa kuwa muhimu zaidi.