Bunge lapewa angalizo  bima ya afya kwa wote

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), kimelishauri bunge kujiridhisha kwanza kama Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote inakidhi matarajio ya wengi kabla ya kuipitisha.

Mwenyekiti wa THTU Taifa, Dk Paul Loisulie alisema hayo wakati wa kuzungumzia mambo matatu ambayo kama serikali inapaswa kuyafanyia kazi ili kutodhoofisha ustawi wa wafanyakazi.

Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa matumaini kwa Watanzania kwamba bunge litapitisha Sheria ya Bima ya Afya kwa wote mwezi huu.

Alisema baada ya Rais Samia kubainisha hatua iliyofikiwa kwenye Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, baadhi ya wananchi wameunga mkono, wengine wakiwa na wasiwasi huku wengine wakidhani mfanyakazi ndiye atakayebebeshwa mzigo wote.

Dk Loisulie alisema kumekuwapo na sintofahamu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, hali ambayo inatokana na  kuwapo kwa tishio la kufilisika na kubadilishwa utaratibu wa wagonjwa wanaotumia bima ya afya kwenye sharti la uhuru wa kwenda kupima afya au kuwaona madaktari ndani ya mwezi mmoja.

Alisema kuwapo kwa lawama kwa wachangiaji wa NHIF kwamba wanatumia vibaya dhana ya bima ya afya kwa kuwaweka wanufaika wasiohusika kwenye orodha inayotakiwa hasa wenye umri mkubwa ambao wanahitaji matibabu zaidi.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vyema kabla ya bunge kupitisha Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, ni vizuri likajiridhisha kwamba itakidhi matarajio ya wengi kwa kiasi kikubwa.

Kuhusu nyongeza ya mishahara, Dk Loisulie alisema THTU pia imeishauri serikali kuangalia namna ya kurekebisha suala la mishahara kwa watumishi wa umma kwa kuweka mikakati ya kuongeza mishahara kwenye bajeti ya mwaka ujao ambayo maandalizi yake yanaanza hivi karibuni.

“Haitapendeza kuwaacha wafanyakazi kwenye kumbukumbu hii isiyo nzuri iendelee kubaki vichwani mwao. Hili linawezekana, tutimize wajibu wetu ili mwaka ujao uwe wa neema,” alisema.

Kuhusu tozo mpya za miamala ya elektroniki, alisema THTU imependekeza kuondolewa na kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x