Bunge lapitisha muswada usimamizi rasilimali za maji

BUNGE leo limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2022.

Akizungumza wakati akifanya majumuisho ya hoja mbalimbali za wabunge wakati wa mjadala wa muswada huo,  Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema kupitishwa kwa muswaada huo kutaimarisha Bodi za mabonde ya Maji katika kusimamia rasilimali za maji nchini.

Pia amesema kutaimarisha uhifadhi wa vyanzo vya maji nchini, ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji nyumbani na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Waziri Aweso aliahidi wizara yake kuendelea kutoa elimu na ushirikishwaji kwa wananchi, kuhusu utunzaji na uhifadhi wa rasilimali.

Awali baadhi ya wabunge wakichangia muswada huo kwa nyakati tofauti, walisema muswada umekuja wakati sahihi, ambapo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya maji, ikiwa kiwango cha rasilimali za maji kiko palepale.

Habari Zifananazo

Back to top button