Bunge latoa maazimio 14 kunusuru mashirika ya umma
Bunge limetoa maazimio 14 kwa lengo la kuongeza uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma kutokana na changamoto zilizoibuliwa katika taarifa za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti & Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa Fedha unaoishia Juni, 2021.
Akiwasilisha maazimio hayo bungeni, Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Japhet Hasunga, maazimio hayo yamejikita katika uwajibikaji na kuimarisha mifumo.
Kuhusu Nakisi ya Ukusanyaji wa Mapato Kupitia Mamlaka ya Mapato, juu ya nakisi ya Sh trilioni 2.81, Bunge limeazimia kuwa Serikali ifanye mapitio ya kina ya mfumo mzima wa ukusanyaji kodi (Comprehensive tax regime review) ili kuhakikisha kodi zote zinakusanywa ipasavyo.
Chombo hicho kinachoisimamia Serikali kimeshauri kufanyika uchunguzi na kuchukua hatua stahiki kwa
Watumishi TRA waliohusika kwa kukadiria kodi chini ya kiwango, kutoshughulikia madeni ya kodi kwa wakati, kuchelewa kusajili mapingamizi ya kodi, kutosimamia ushuru wa forodha kwenye bidhaa za mafuta.
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)/Mwendokasi
-Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aombwe kufanya ukaguzi maalumu (Special audit) wa malipo ya fidia kiasi cha Sh bil 1.0, usumbufu Sh. Milioni 434 yaliyofanyika DART.
Kuungua Soko la Kariakoo
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, afanye ukaguzi wa kiuchunguzi (Forensic audit) wa Shirika la Masoko Kariakoo ili kubaini iwapo kuna ubadhirifu wa
fedha za umma uliofanyika na kufichwa baada ya soko kuungua.
Vyombo vya Dola vianze uchunguzi wa uliokuwa uongozi wa Soko la Kariakoo kubaini iwapo walihusika na jinai katika kuficha nyaraka za fedha kwa wakaguzi.
Stika bandia
Serikali ichukue hatua za kisheria kwa watumishi 32 wa Idara ya Uhamiaji waliotajwa kuhusika katika mauzo ya stika viza bandia katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kwa kuzingatia uhusika wa kila 1 na matokeo ya ukaguzi maalumu.
Ubadhirifu Tanesco, REA
Ubadhirifu, pamoja na hatua za kisheria na kinidhamu kwa watumishi wa REA na TANESCO waliohusika kusimamia mradi wa REA awamu ya Pili mkoa wa Mara kwa kutotimiza majukumu yao.
Serikali ichukue hatua za kisheria kwa mkandarasik ampuni ya DERM Electrics (T) Limited kwa udanganyifu.
Kuhusu hali ya Ukwasi TPDC, TANESCO na STAMICO)
-Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, iongeze mtaji katika mashirika ya mkakati ya Serikali kwa kufanya marekebisho ya msingi katika madeni ya Taasisi hizo ili kuyageuza kuwa mtaji (Equity).
Serikali ichukue hatua stahiki za kisheria kwa mkandarasi aliyechelewesha kukamilika ujenzi wa gati la kuegeshea meli katika bandari ya Mtwara.
-Serikali ichukue hatua stahiki kwa Watumishi wa Wizara ya Nishati, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango na TANESCO walioshiriki katika mchakato mzima wa uingiaji, usimamizi, utekelezaji na uvunjaji wa mkataba kati ya TANESCO na Symbion.
Kuhusu Dosari Katika Usimamizi wa Mikataba na Athari zake katika Matumizi ya Fedha za Umma; Bunge limeazimia kuwa Serikali ifanye uchunguzi kubaini iwapo riba zilizotokana na mikataba ya ujenzi wa barabara katika TANROADS zilikuwa na uhalali na ulazima wa kuwepo.
Aidha, Bunge limeazimia kuwa ili kuabiliana na uhaba wa dawa na kuharibika kuharibika;
– MSD isiagize dawa, vitendanishi au chanjo ambazo muda wake wa matumizi upo chini ya miezi sita
-Kusambaza dawa siku 30 baada ya malipo
-Kutoa taarifa ndani ya saa 24 ikiwa dawa hakuna