Bunge latoa pole ajali ndege ya Precision Air

Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba baada ya kutokea ajali ya ndege ilioua jumla ya watu 19 Bukoba, Kagera.

Spika Dk Tulia Ackson ametoa pole hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha sita cha Mkutano wa Tisa wa Bunge jijini Dodoma leo Jumatatu asubuhi.

Amezitaka mamlaka husika kuendelea kufuatilia zaidi juu ya ajali hiyo.

Advertisement

“Waheshimiwa wabunge, kama mnavyofahamu, jana Jumapili majira ya saa mbili asubuhi kulitokea ajali ya ndege inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Precision Air ambayo ilitua katika Ziwa Victoria takribani mita 100 kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, mkoani Kagera,” amesema Spika Tulia.

Kabla ya kuanza kujibu maswali Bungeni, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),  Patrobas Katambi ameungana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa wafiwa.

Jana Rais Samia alitoa salamu za pole kwa walioguswa na tukio hilo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *