PARIS; Ufarasansa; RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametangaza kuvunjwa kwa Bunge la taifa na kuandaa uchaguzi mpya wa wabunge, baada ya ushindi katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya.
“Nitaweka saini rasmi katika muda mfupi agizo la kuitisha uchaguzi wa wabunge ambao utafanyika Juni 30 kwa duru ya kwanza na Julai 7 kwa duru ya pili,” aMEsema Rais Macron.
Tangazo hili alilitoa kupitia televisheni ya taifa nchini humo baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya, “matokeo sio mazuri kwa vyama vinavyotetea Umoja wa Ulaya”.