JAMAICA: FAMILIA ya Peter Anthony Morgan (Peetah), mwimbaji kiongozi wa bendi maarufu ya reggae, Morgan Heritage imetangaza kuwa mwimbaji huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 46.
Katika taarifa iliyotolewa na familia hiyo inasema kwamba Peter aliaga dunia siku ya Jumapili lakini haikusema chochote kuhusu chanzo cha kifo cha Peetah.
Peter, anayejulikana sana kama Peetah, aliunda Morgan Heritage na kaka zake mnamo 1994 nchini Jamaica, akiwa na ndugu zake wanne na aliiongoza bendi hiyo kutwaa tuzo ya Grammy ya albamu bora ya reggae mnamo 2016 kupitia albamu yao ya Strictly Roots.
Hapa Tanzania watakumbukwa kupitia nyimbo ya “Hallelujah” waliyoshirikishwa na Diamond Platinumz kutoka WCB.