MSANII wa Nigeria ‘Burna Boy’ amechaguliwa kutumbuiza kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Atatürk Olympic-Istanbul, Uturuki Juni 10, 2023.
Taarifa ya msanii huyo kutumbuiza kwenye mchezo wa fainali imetolewa na Shirikisho la Soka Ulaya ( UEFA) kupitia tovuti na mitandao yao ya kijamii
“Mimi mwenyewe kama shabiki mkubwa wa soka, najua haijawa kubwa zaidi ya UEFA Champions League! Ndiyo maana ninafuraha sana kutumbuiza kwenye jukwaa la Pepsi kwenye fainali ya mwaka huu”. Amesema Burna Boy
Amesema “Muziki na soka ni mchanganyiko wa mwisho, kwa hivyo tayari unajua nitakuwa nikileta shangwe na kufanya maajabu huko Istanbul”.ameongeza