Burundi,Tanzania wakubaliana kuibua vipaji vya vijana

TAASISI mbili za kukuza, kuibua na kuendeleza soka kwa vijana kutoka Tanzania na Burundi zimeingia makubaliano maalum ya ushirikiano wa kuibua na kuendeleza vipaji vya soka vya vijana .

Future stars academy kutoka Arusha imeingia makubaliano na taasisi ya michezo ya Didier Drogba academy kutoka jijini Bujumbura, Burundi zimetia saini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya soka miongoni mwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Sote tunafanya kazi ili kuhakikisha kwamba wanasoka chipukizi na wanaochipukia Afrika Mashariki wanatimiza ndoto zao za kuwa wanasoka wa kimataifa ” ameeleza Mkurugenzi wa Future Stars Academy (FSA), Alfred Itaeli.

Amesema taasisi ya Future stars inajihusisha na kufundisha soka vijana wenye umri wa kuanzia miaka 4 hadi wachezaji wa chini ya miaka 20 .

“Wao wametembelea na kuona jinsi tunavyoza vipaji kwa malengo ya ujumla na tunaamini kupitia mashindano ya vijana Afrika mashariki ‘chipkizi Cup ‘ni njia mojawapo ya kuweza kuwapatia vijana fursa ya kutimiza ndoto za kuwa wachezaji kimataifa kutokana na kuwa mawakala mbalimbali hufika na kuangalia vipaji,”ameongeza Itaeli.

Kwa upande wake kiongozi wa Didier Drogba Academy, Nshimirimana Djuma amesema taasisi yao imekuwa ikitaka kushirikiana na Future Stars na Kwa kuanzia wataanza kuleta wachezaji mwezi Julai nchini Tanzania.

“Kwa kweli, mwaka jana tulitamani hata kushiriki michuano ya ‘Chipkizi Cup 2023,’ jijini Arusha lakini tulichelewa kidogo na hatukuwa na muda wa kutosha wa maandalizi ,” amesema Djuma.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Djuma, mwaka huu, taasisi yao ya Didier Drogba ina mpango wa kuleta Arusha timu nne za soka za vijana katika makundi kadhaa, ikiwemo ya miaka 6 hadi 9; Miaka 10 hadi 13; Miaka 14 hadi 16 na miaka 17 hadi 18.

“Tunashukuru haya makubaliano ya miaka miwili na mwezi wa Saba tutaanza kuleta wachezaji na sisi tulianza kufundisha soka vijana mwaka 2017 na Kwa sasa tuna vijana 145 hivyo programa hii tunaimani vijana watapata fursa ya kuonekana zaidi kimataifa,”amefafanua Djuma.

Taasisi ya soka ya Future Stars imekuwa ikiandaa Mashindano ya kila mwaka ya vin ana kwa nchi za Afrika Mashariki na nje yanayojulikana kama ‘Chipkizi Cup.’

Habari Zifananazo

Back to top button