Bwana harusi ajinyonga akisubiriwa ukumbini

SWADIKA Abasi (50), mkazi wa Kiseke katika Manispaa ya Ilemela amejinyonga hadi kufa kwa mtandio sebuleni kwake baada ya kujifunga na kujining’niza kwenye kenchi la paa la nyumba yake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wibroad Mtafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 17, mwaka huu, saa 5.45, Mtaa wa Zenze, Kata ya Kiseke katika Manispaa ya Ilemela.

Alisema ilidaiwa Swadika alikuwa akiishi na mkewe aitwaye Elieth Rwegoshera (40) ambaye pia ni mkazi wa Kikseke-Ilemela waliyekuwa wametoka kufunga ndoa siku hiyo ya Desemba 17, majira ya saa moja katika msikiti wa Swadikil Amiin Kiseke.

Alisema baadaye walitarajia kwenda kufanya sherehe fupi katika ukumbi wa Mtena B ulioko Buzuruga. Hata hivyo, hadi saa nne usiku mwanamume huyo aliyekuwa akisuburiwa hakutokea ukumbini.

“Ilibidi sasa atafutwe na walipokwenda nyumbani kwake walikuta amejinyonga kwa mtandio huku mwili wake ukiwa umening’inia kwenye kenchi,” alisema.

Kamanda Mtafungwa alisema katika uchunguzi wa awali walipatikana kipande cha karatasi chenye ujumbe wa kujiua unaohifadhiwa kwa sasa kwa ajili ya upelelezi na uchunguzi. Hata hivyo, Kamanda hakutaja ujumbe huo ulihusu nini.

Aliwataka ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa watulivu wakati polisi wakiendelea na upelelezi wa tukio hilo.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure kwa uchunguzi wa kitalaamu,” alisema.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
scola novath
scola novath
5 months ago

Matukio ya mwanza na kagera yanafanya niamini kuwa jamii yake inahitaji Elimu ya hali ya juu katika uchambuzi wa kufikiria kabla ya kufany tukio!!! yani matukio ya kiukatili yanayoendelea katika jamii hiyo yanatisha! nguvu ya ziada inahitijika katika kufatilia changamoto za kifamilia na kijamii tukiachana na kukazania kukabili suala la kupinga ukatilivwa jinsia (Ke).

jamii inaamini kuwa ukatili wa kijinsia ni upande Ke tu lakini vipi kuhusu unyanyasajii baina ya familia na familia!???

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x