Bwawa la Nyerere kuanza kunguruma Januari

DAR ES SALAAM: SERIKALI inatarajia kuwasha kinu cha kwanza cha kufua umeme mwezi Januari, 2024 katika bwawa la Nyerere (JNHPP) ikiwa ni jitihada za kuzalisha umeme wa kutosha ambao ni muhimu kwa wazalishaji.

 

Rais Samia ametanabahisha hayo mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki.

Advertisement

“Pamoja na jitihada nyingine za gesi, sola na mambo mengine, lakini katika umeme wa ‘hydro’ maji tunategemea nadhani katikati ya mwakani malalamiko mengi yatakuwa yamepungua,” amesema Rais Samia.

Aidha, Mkuu huyo wa nchi amesema uwashwaji wa kinu cha kwanza utafuatiwa na uwashwaji wa kinu cha pili mnamo Aprili, 2024 lengo ni kuhakikisha umeme nchini unakuwa wa uhakika hivyo kuongeza uzalishaji.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *