‘Bwawa la Nyerere limeonesha tunaweza kufanya makubwa’

‘RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) uliopo Rufiji mkoani Pwani, umeonesha kuwa Watanzania wanaweza mambo makubwa.

Amesema mradi huo unatoa taswira kuwa Tanzania inaweza kufanya mambo makubwa kwani unapotaja mabwawa makubwa, hilo la Julius Nyerere lipo.

Ametoa kauli kauli hiyo wakati akihutubia kwenye sherehe ya uzinduzi wa ujazaji maji katika bwawa la kufua umeme kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) uliopo Rufiji mkoani Pwani, baada ya hatua ya kujenga tuta linalosaidia uhifadhi wa maji katika bwawa hilo kukamilika.

Advertisement

Rais Samia amefanya uzinduzi huo katika hafla iliyofanyika eneo la mradi kwa kubonyeza kitufe kilichoshusha mageti yatakayoziba njia ya mchepusho wa maji na kuruhusu maji kuanza kujaa katika bwawa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *