CAF yairudisha Yanga Tunisia

CAF yairudisha Yanga Tunisia

YANGA imerudishwa tena Tunisia. Pengine ndivyo unavyoweza kusema kwa kifupi ukizungumzia droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyochezeshwa leo.

Ndiyo Yanga imerudishwa Tunisia, ambapo imepangwa Kundi D la michuano hiyo pamoja na timu ya Monastir ya Tunisia, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Real Bamako ya Mali.

Yanba ilifuzu hatua ya makundi baada ya kuitoa Club Africain ya Tunisia kwa bao 1-0 mjini Tunis, Tunisia baada ya timu hizo kutoka 0-0 Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Advertisement

Kundi A la michuano hiyo kuna timu za USMA Alger ya Algeria, Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Al Akhder ya Libya na St Eloi Lupopo ya DRC, huku tTimu za Kundi B ni ASEC Mimosas ya Ivory Coast, DC Motema Pembe ya DRC, Diables Noirs pia DRC na Rivers United ya Nigeria.

Timu za Kundi C ni Pyramids na Future za Misri, ASKO Kara ya Togo na AS FAR Rabat ya Morocco.