CAG abaini dawa zilizoisha muda wake MSD

RIPOTI ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini uwepo wa dawa zilizoisha muda wake katika Bohari Kuu ya Dawa kabla ya kusambazwa zenye thamani ya sh milioni 235.84.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo Aprili 6, 2023 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Charles Kichere amesema udhaifu huo unatokana na udhibiti duni wa mfumo katika kuthibitisha muda wa kuharibika kwa dawa au vifaa tiba.

Akitoa ripoti hiyo CAG Kichere amesema kuwa pia ofisi yake ilibaini kuwepo kwa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 976.58 vikiwa vimeisha muda wa matumizi.

Advertisement

“Pia nilibaini hospitali za rufaa 17 zilihifadhi dawa za matibabu zilizoisha muda wake zenye thamani ya shilingi bilioni 2.24 na hizo zimekaa kwa wastani wa miezi mitatu hadi miaka 10, baadhi ya hospitali hizo ni Benjamin Mkapa, Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara (Ligula, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya”. CPA Charles Kichere,